Fiorentina yapunguza kasi ya SPAL

67

Fiorentina imekamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya Italia baada ya kuharibu mwanzo mzuri wa msimu wa SPAL kwa ushindi wa 3-0

SPAL ilikuwa katika nafasi ya pili pointi tatu nyuma ya mabingwa Juventus kabla ya mechi hiyo, huku wakiwa wamefungwa bao moja tu katika mechi nne. SPAL sasa wameshuka hadi nafasi ya tano.

Winga wa zamani wa Arsenal Gervinho alifunga bao safi wakati Parma iliilaza Cagliari 2-0. Parma ambao waliwashangaza Inter Milan wikendi iliyopita sasa wamepanda hadi nafasi ya saba.

Author: Bruce Amani