Fortuna yaionjesha Dortmund kichapo cha kwanza

Fortuna Duesseldorf iliwaduwaza Borussia Dortmund na ushindi wa 2-1 Jumanne, kikiwa ni kichapo chao cha kwanza katika Bundesliga msimu huu.

Mabao kutokakwa Dodi Lukebakio na Jean Zimmer katika kila nusu ya mchezo yaliupunguza uongozi wa Dortmund hadi pointi sita dhidi ya Borussia Moenchengladbach, ambayo awali iliizaba Nuremberg 2-0. Bayern Munich ambao wako nyuma na tofauti ya pointi tatu watacheza leo Jumatano dhidi ya RB Leipzig.

Paco Alcacer aliifungia Dortmund bao lake la 12 katika Bundesliga msimu huu katika dakika ya 81, lakini Duesseldorf ikapambana na kupata ushindi wao wa pili mfululizo, wao wa nne msimu huu na wao wa kwanza dhidi ya vinara hao wa ligi katika miaka 22. Sasa wameondoka katika eneo la kushushwa ngazi.

“Inapendeza sana kuwa timu ya kwanza kuizaba Dortmund msimu uu, lakini kama tu itakuwa pointi tatu,” Alisema kocha wa Duesseldorf Friedhelm Funkel.

Galdbach yaongeza shinikizo

Moenchengladbach iliiwekea shinikizo Dortmun kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya timu iliyopandishwa daraja Nuremberg. Thorgan Hazard alishindwa kufunga penalti lakini akarekebisha kosa hilo kwa kufunga bao la kwanza baada ya kipindi cha kwanza na Alassane Plea akafunga kazi kwa kutia kimyani bao lake la tisa msimu huu. Nuremberg huenda ikashika mkia kama Hannover itaishinda Freiburg leo. Ijumaa Gladbach watacheza na Dortmund.

Katika matokeo mengine, Augsburg walitoka sare ya 2-2 na Hertha Berlin na Wolfsburg wakawazaba Stuttgart 2-0.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends