Frankfurt waibwaga Arsenal na kumuongezea Emery mbinyo

64

Eintracht Frankfurt ilipata ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Arsenal mjini London, katika mchuno wa hatua ya makundi wa Ligi ya Europa jana usiku. Arsenal walitangulia kufunga bao katika kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wa Gabon Pierre-Eemric Auabameyang kabla ya Frankfurt kutoka nyuma na kuponyoka na ushindi kupitia mabao ya kipindi cha pili yaliyotiwa kimiani na Daichi Kamada. Kama Frankfurt watapata ushindi katika mechi yao ya mwisho mbele ya mashabiki wa nyumbani dhidi ya washika mkia kwenye Kundi lao Vitoria, watajikatia tiketi ya hatua ya mchujo kwa msimu wa pili mfululizo.

Kwingineko, bao pekee la Lars Stindl lilitosha kuipa Borussia Mönchengladbach ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Wolfsberg na kuwaweka kileleni m,wa kundi lao kabla ya mechi za mwisho za hatua ya makundi. Gladbach itaialika Istanbul Basaksehir katika mechi yao ya mwisho na lazima iepuke kichapo ili ilufuzu. Wolfsburg won ilishinda 1-0 ugenini dhidi ya Oleksandriya na kutinga hatua ya mchujo.

Author: Bruce Amani