Galatasaray ina matumaini ya kumnyakua mshambuliaji wa Nigeria

178
Mashabiki wa timu ya Galatasary wana matunaini kuwa Henry Onyekuru huenda akarudi kilabuni hapo baada ya kutoka Monaco. Hiyo ni baada ya timu ya Monaco kumfurusha kocha wake Roberto Moreno wiki iliyopita.
Moreno alikuwa na matumaini na Henry na kumpa kipaumbele katika washambulizi aliotaka kufanya nao kazi katika msimu ujao.
Lakini Moreno akapigwa kalamu na Monaco kwa sasa,  mashabiki wa Gala wamemwambia mkuu wa kilabu kuanza mazungumzo na wakala wa Onyekuru.
Uongozi wa Galatasaray unamfuatilia kwa karibu mshambulizi huyo.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Everton alirejea Monaco mapema Julai kuanza mazungumzo juu ya hatma yake baada ya mkataba wake kumalizika Julai 1. Henry alirudi Galatasary kwa mkopo kutoka Monaco.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 22, alishindwa kuonyesha makali yake baada ya kutoka Everton ya England.

Author: John Major Ouma