Ivan Gazidis aiaga Arsenal

53

Arsenal imesema afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis anaondoka klabu hiyo ya England ili kujiunga na AC Milan ya Italia. Gazidis amekuwa katika klabu ya Arsenal inayomilikiwa na bwenyenye wa Kimarekani Stan Kroenke. Arsenal imesema kujiuzulu kwa Gazidis kutakamilishwa Oktoba 31.

Kampuni ya Arsenal Holdings Plc imesema Raul Sanllehi, ambaye sasa ni mkuu wa mahusiano ya kandanda, atakuwa mkuu wa kandanda, na afisa mkuu wa kibiashara Vinai Venkatesham atakuwa meneja mkurugenzi.

Author: Bruce Amani