Ghana mwenyeji wa AFCON 2018 kwa wanawake

50

Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika, CAF imeidhinisha rasmi Ghana kuwa mwenyeji wa fainali za Afrika kwa wanawake.

Awali kulikuwa na uvumi kuwa CAF imeiondoa Ghana kuandaa fainali hizo lakini kamati ya utendaji iliyokutana katika Mji wa Sham El Sheikh nchini Misri imesema kwamba shirikisho hilo linapaswa kuisaidia Ghana kikamilifu ili ifanikishe mchakato wa kuandaa fainali hizo.

Fainali hizo zitaanza Novembva 17 hadi Disemba 1 mwaka huu ni zitakuwa fainali za 13 tangu kuasisiwa kwake.

 

 

Author: Bruce Amani