Ghana yabanwa mbavu na vibonde Benin

Timu ya taifa ya Ghana Black Stars imebanwa mbavu na Benin katika mchezo wa kundi F wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019 uliomalizika kwa sare ya 2-2 uliofanyika Juni 25 Jumanne usiku.

Black Stars wakiwa mabingwa mara nne (4) wa AFCON walijikuta wakitanguliwa kwa goli la mapema dakika ya pili kabla mambo kukaa sawa baada ya kusawazisha na kisha kuongoza kisha kupoteza uelekeo kwa mara ya pili.

Iliwahitaji Benin dakika 2 kutangulia kwa goli la Mickael Pote kabla ya Andrew Ayew kusawazisha goli dakika ya 9.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Ghana ambao walipata goli la pili kupitia kwa kaka mdogo Jordan Ayew dakika ya 42 kabla ya John Boye kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 54 kisha Mickael Pote kunako dakika ya 62 kusawazisha goli, likiwa goli lake la pili la mchezo.

Kundi F

Cameroon -3
Benin -1
Ghana -1
Guinea-Bissau-0

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends