“Ghost” arejea tena kama kocha wa Harambee Stars

Shirikisho la Kandanda Kenya –FKF limemtambulisha Jacob “Ghost” Mulee kuchukua usukani wa timu ya taifa ya kandanda ya Harambee Stars. Mulee ametangazwa saa chache tu baada ya kocha Francis Kimanzi kujiuzulu. Mulee anarudi usukani baada ya kuiongoza Harambee Stars katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2004 iliyoandaliwa Tunisia:

Kimanzi na wasaidizi wake wawili alijiuzulu Jumanne, wiki chache tu kabla ya kuanza mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2021.

Kimanzi ambaye alikuwa msaidizi wa Mfaransa Sebastien Migne wakati Kenya ilifuzu kwamichuano hiyo kwa mara ya kwanza katika miaka 15 mnamo mwaka wa 2019, aliondoka kwa “maelewano ya pande mbili”

Kenya itawaalika Comoros katika mechi ya Kundi G wiki z´tatu zijazo. Kenya ipo katika nafasi ya pili, na pointi mbili, nyuma ya Comors, ambao wanaongoza kundi G na pointi nne. Misri na Togo pia zipo kwenye kundi hilo.

Author: Bruce Amani