Giroud atua rasmi Milan, apewa jezi namba 9

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud amekamilisha uhamisho wa kujiunga na AC Milan kwa ada ambayo haijawekwa bayana kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Mchezaji huyo alijiunga na The Blues mwaka 2018 mwezi Januari akitokea Arsenal kwa ada ya pauni milioni 18.
Giroud, 34, aliishukuru klabu ya Chelsea kwa namna ambavyo wametumia kipindi chao pamoja kwa mafanikio makubwa.
Aliandika: “Ushindi wa pamoja wa Kombe la FA, Ligi ya Europa na Ligi ya Mabingwa Ulaya, hautasaulika kwangu”.
Usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz na Timo Werner ulikuwa mchungu kwa Giroud ambaye muda wa kucheza ulipungua maradufu katika msimu wa 2020/21.
Kwa ujumla wake alifunga bao 39 katika mechi 119 ndani ya Chelsea.
AC Milan walimaliza alama 12 pungufu ya bingwa wa Seria A klabu ya Inter Milan msimu uliomalizika karibuni.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares