Giroud atupia, Milan ikishinda na kwenda kileleni

201

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea Olivier Giroud amefunga goli pekee kwenye ushindi walioupata AC Milan dhidi ya Torino katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A mtanange uliopigwa Leo Octoba 26,2021.

Ushindi wa Milan umekuwa muhimu baada ya kuipeleka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa Serie A kwa tofauti ya alama tatu.

Giroud, 35, ambaye ni nyota wa kimataifa wa Ufaransa alifunga bao akimalizia kazi nzuri ya Rade Krunic kunako dakika ya 14 ya mchezo.

Giroud mpaka sasa amefunga goli nne katika mechi sita za Ligi ambapo goli zote nne amezifunga katika dimba la San Siro, itakumbukwa Giroud alijiunga na AC Milan kutokea Chelsea baada ya mkataba kumalizika.

Milan watakuwa na kibarua kizito kutoka kwa AS Roma ya Jose Mourinho siku ya Jumamosi.

Author: Bruce Amani