Giroud awashukuru Chelsea, kujiunga na Milan

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Olivier Giroud ameishukuru klabu ya Chelsea kwa kumbukumbu nzuri ambazo zimetokea katika kipindi ambacho alikuwa Stamford Bridge.

Kwa kheri ya Giroud inakuja kipindi ambacho ametua viunga vya San Siro ndani ya klabu ya AC Milan inayoshiriki Ligi Kuu Serie A.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, anategemewa kumwaga wino wa miaka miwili, mwishoni mwa wiki hili dili lake litakamilika.

Kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa mchezaji huyo ameandika kuwa “Naanza safari mpya yenye mwangaza na moyo wenye furaha”.

“Ushindi wetu kwenye Kombe la FA, Ligi ya Europa na Ubingwa wa Ligi ya Ulaya si wakusahaulika kwangu”, aliandika mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal.

Giroud alijiunga na Chelsea kutokea Arsenal mwaka 2018 mwezi Januari kwa ada ya pauni milioni 18 ambapo aliongeza kandarasi mpya ya mpaka 2022.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares