Giroud, Griezmann watupia Ufaransa ikiichapa Bulgaria

Timu ya Taifa ya Ufaransa imeendelea kuwa kwenye ubora mkubwa katika mechi za maandalizi ya michuano ya Euro 2020 baada ya kufanikiwa kuondoka na bao tatu mbele ya Bulgaria.
Ufaransa ambao ni mabingwa wa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi wanaingia kwenye michuano hiyo kama wababe wa dunia wenye kipaumbele cha kubeba taji hilo.
Magoli yakawekwa kimiani na mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann akifunga bao la aina yake, mshambuliaji wa Chelsea Oliver Giroud akitokea benchi aliingia kambani mara mbili.
Kocha Didier Deschamps alianza na Kylian Mbappe, Griezmann na Karim Benzema katika eneo la ushambuliaji ambalo mwisho wa siku wakazalisha magoli matatu.
Ufaransa itaanza kampeni ya kuwania taji la Euro 2020 kwa kucheza na Ujerumani kabla ya kupepetana na Hungary na kumaliza na Ureno Juni 23.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares