Goli la Vardy laipeleka Leicester City hatua ya mtoano Ligi ya Europa

348

Jamie Vardy alifunga goli moja kwenye dakika za lala salama lililoipeleka hatua ya 16 bora katika mashindano ya Ligi ya Europa dhidi ya Braga. Akiingia kama mchezaji wa akiba wakati huyo Leicester City ikiwa nyuma kwa goli 3-2, Vardy alitumia vyema pasi ya mlinzi wa pembeni Marc Albrighton kukwamisha  mpira nyavuni na mechi kumalizika kwa sare ya goli 3-3.

Al Musrati aliwatanguliza Braga kabla ya Harvey Barnes kusawazisha ingawa dakika chache tena wenyeji wa mchezo huo wakatangulia kwa goli la Paulinho. Luke Thomas akaweka mzani sawa kwa kufunga la pili kufanya mambo kuwa 2-2. Bao la Fransergio lilionekana kama linaipa ushindi Braga na kutoka kusikojulikana Jamie Vardy akaingiza wavuni na kuufanya mchezo huo kuisha kwa sare hiyo. Ushindi wa goli 3-0 wa Zorya Luhansk mbele ya AEK Athens ulimaanisha kuwa kikosi cha kocha Brendan Rodgers kilihitaji alama moja tu kuingia mtoano

Author: Asifiwe Mbembela