Gomes ajitapa kuwa Simba ni Bora Afrika Mashariki

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa ameweka wazi kuwa msimu huu kikosi hicho kimekuwa bora si Tanzania pekee bali Afrika Mashariki nzima na ndiyo maana imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo.

 

Gomes amesema kikosi ni bora kulinganisha na vingine ndani ya ukanda huu na ndiyo sababu inayopelekea kushinda mechi nyingi hali kadhalika magoli mengi pia yamefungwa.

 

Aidha, ameupongeza uongozi wa klabu chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kwa kumuwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa muda wote tangu atue nchini.

 

“Simba ni timu bora kwa sasa Afrika Mashariki nzima nadhani baada ya muda tutacheza fainali ya Afrika. Ukiangalia msimu huu tumefunga mabao mengi na tumeshinda mechi nyingi pia,” amesema Gomes.

 

Gomes amesema ana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili ijayo Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

“Dhamira yetu ni kuhakikisha tunachukua na taji la FA na ninatumaini tutafanikisha hilo,” amesma Gomes.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares