Gor Mahia Kuwavaa Homeboyz Dimba la Kasarani

29

Kifungo cha takribani miezi mitatu ya kutotumia uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Gor Mahia kimemalizika na sasa timu hiyo imeruhusiwa kuendelea kutumia uwanja huo.

Gor Mahia ambao ni mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu nchini Kenya walizuiwa kutumia uwanja wa Kasarani kufuatia mashabiki wa timu hiyo kusababisha vurugu kwenye mechi yao na Vihiga Bullets siku zaidi ya siku 90 zilizopita.

Katika kipindi chote hicho, K’Ogalo wamekuwa wakitumia viwanja mbalimbali kama dimba la Moi, Kisumu ambapo mechi ya kwanza kuchezwa uwanja wa nyumbani itakuwa Jumamosi Mei 21 dhidi ya vinara Kakamega Homeboyz.

Kwa sasa Gor Mahia wako kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo wa KPL wakiwa na mechi 30 alama 47 pointi 12 nyuma ya Homeboyz.

“Tunapenda kuthibitisha kuwa adhabu yetu imeondolewa rasmi na sasa mechi zetu zote zitaanza kuchezwa uwanja wa Kasarani”, alisema Meneja wa timu hiyo Jolawi Obondo.

Author: Bruce Amani