Gor Mahia wapoteza mechi yao ya kwanza msimu huu

Mabingwa wa ligi kuu ya kandanda nchini Kenya – KPL Gor Mahia walipoteza mechi yao ya kwanza msimu huu baada ya kunyukwa 1-0 na Mathare United katika uwnaja wa Machakos.

Goli la Dennis Otieno katika dakika ya 89 lilisaidia vijana hao wa mtaa wa mabanda kunyakua alama tatu.  KO’gallo wanasalia katika nafasi ya pili alama moja nyuma ya vinara Tusker  huku wakiwa na mechi moja mkononi. Katika mechi nyengine Bandari walinyukwa 3-1 na Western Stima mjini Kisumu na kusalia katika nfasi ya 10.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends