Gor Mahia Yaweka Rehani Ubingwa FKFPL, Yatoa Sare na Posta Rangers

184

Matokeo ya sare ya bao 2-2 ambayo vinara wa Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL Gor Mahia wameyapata dhidi ya Posta Rangers yameifanya sasa kusalia kileleni kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Tusker FC ambao wana mchezo mmoja mkononi.

Katika mchezo uliochezwa uwanja wa Nyayo, Gor Mahia walifufunga magoli mawili kupitia kwa Benson Omala katika ungwe ya kwanza lakini wakashindwa kulinda ushindi huo na kufanya Posta kusawazishiwa magoli hayo kupitia kwa Calvin Odongo na bao la kujifunga la Gad Mathew.

Kocha wa Gor Mahia Johnathan McKinstry akizungumzia mchezo huo amesema hajawai kuona mchezo mbovu kama huo tangia kuanza kuinoa timu hiyo ambayo ndiyo mabingwa wa kihistoria wa Ligi wakitwaa mara 19.

Author: Asifiwe Mbembela