Gor yamenyana na Nyasa Big Bullets

275

Mabingwa watetezi wa ligi ya soka nchini Kenya, KPL Gor Mahia leo alasiri wanashuka dimbani dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mkondo wa pili wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mechi hiyo itang’oa nanga saa tisa unusu katika uwanja wa Kamuzu Banda mjini Blantyre, Malawi. Gor Mahia walishinda mechi ya mkondo wa kwanza goli 1-0 na leo wanahitajia ushindi au sare kufuzu katika hatua ya makundi.

Kikosi cha Gor Mahia kitakuwa bila ya mchezaji nyota Francis Kahata. Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amedokeza kuwa Kahata anaelekea kujiunga na klabu ya Constantine ya Algeria. “Baada ya kushauriana na wakala wake pamoja na klabu ya Constantine tumeona hakuna haja tumchezeshe kwa sababu kule anakokwenda pia atacheza mechi hizo!” Ambrose Rachier.

VIKOSI;

Nyasa Bullets

Kikosi cha kwanza: Kakhobwe; Lanjesi (C), Gabeya, Zonda, Fodya; Kayira, Kabichi, Kangunje, Mgwira, Righteous; Msowoya

Benchi: Chiyenda, Mkandawire, Kumwenda, Maunde, Mkwate, Kondowe, Munthali

Kikosi cha kwanza: 

29-Boniface Oluoch, 26. Philemon Otieno, 6. Shafiq Batambuze, 12. Joash Onyango, 18. Haron Shakava, 20. Earnest Wendo, 3. Samuel Onyango, 30. Humphrey Mieno, 25. George Odhiambo, 23. Francis Mustafa, 22. Erisa Ssekisambu

Bench: 1. Frederick Odhiambo, 27. Charles Momanyi, 5. Pascal Ogweno, 17. Benard Ondiek, 10. Cercidy Okeyo, 24. Lawrence Juma, 11. Boniface Omondi

Author: Bruce Amani