Gor yawakata Chui kucha katika mtanange wa watani wa jadi

Kiungo wa Gor Mahia Lawrence Juma, anadai ushindi wao wa 4-1 dhidi ya watani wao wa jadi AFC Leopards jana Jumapili kuliwapiga jeki na kuwapa fursa nzuri ya kuendeleza matokeo mazuri.

 

KO’gallo walibanduliwa nje ya michuano ya shirikisho barani Afrika na klabu ya DC Motema Pembe ya Congo kabla ya kunyukwa 1-0 na Mathare United katika ligi ya KPL Jumatano. Lawrence yuko katika kikosi cha Harambee Stars kitakachocheza na Misri katika mechi ya kufuzu mashindano ya AFCON.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends