Greenwood ajifunga Manchester United mpaka 2025

Mshambuliaji wa kimataifa wa England na klabu ya Manchester United Mason Greenwood ameongeza kandarasi ya kuendelea kusalia ndani ya United mpaka mwaka 2015 kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba mwingine.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza ngazi ya wakubwa taifa mwaka Jana Septemba, mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2023.

Greenwood ni zao halisi la United, amekuwa na timu hiyo tangia akiwa na umri wa miaka 7, amefunga goli 21 katika mechi 82, alicheza mechi yake ya kwanza kwa Mashetani Wekundu mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 156.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares