Griezmann arejea Atletico kutokea Barca

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga Atletico Madrid imemsajili tena mshambuliaji wa Kifaransa Antoine Griezmann kutokea Fc Barcelona kwa mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo.

Atletico watakuwa wanamlipa mchezaji huyo mshahara ambapo kuna kipengele cha kumsajili moja kwa moja baada ya kandarasi yake ya mkopo wa mwaka mmoja kumalizika.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, alifunga goli 133 katika mechi 257 akiwa Atletico kabla ya kuondoka na kujiunga na Barcelona kwa dau la pauni milioni 107 2019, akiwa Barca amefunga goli 35 katika mechi 102 akishinda taji moja pekee.

Anakuwa mchezaji wa 11 kuondoka Barcelona kutokana na changamoto ya kifedha ukijumulisha na staa wa Argentina na Paris St-Germain kwa sasa Lionel Messi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares