Haaland aiokoa Dortmund kukutana na kipigo kutoka Augsburg

296

Borussia Dortmund imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-3 dhidi ya Augsburg katika mchezo wa Bundesliga uliopigwa leo Jumamosi.

Kinda Erling Braut Haaland ameingia katika historia nyingine baada ya kuingia kutokea bechi na kufunga goli tatu za haraka zilizoipa alama tatu Dortmund ambayo ilianza vibaya mtanange huo wa leo kwa kufungwa goli 2-0.

Kinda huyo aliyejiunga na Dortmund kwa dau la paundi milioni 17 baada ya kufunga goli 28 kwenye mechi 22 akiwa Red Bull Salzburg, akifunga hatrick tano katika goli hizo.

Haaland aliingia kunako dakika ya 56 wakati Dortmund wamefungwa goli 3-1, akafunga dakika tatu baadae, akafuatia Jordan Sancho kuweka mambo kuwa 3-3.

Baadae kinda huyo aliongeza goli mbili na kufanya tamati ya mchezo huo kuwa 5-3 Augsburg wakilala na viatu baada ya shughuli pevu ya Haaland.

Huenda goli tatu alizozifunga leo Haaland zikaimua zaidi Juventus, Manchester United baada ya kuhusishwa kumsajili kabla ya dili zao kuishia njiani, leo zitajutia kuwa heri angezifungia klabu zao.

Augsburg waliongoza 2-0 kupitia goli za Florian Niederlechner na Marco Richter, kabla ya Julian Brandt kufunga goli moja upande wa Borussia Dortmund dakika za awali kipindi cha kwanza, Borussia licha ya ushindi bado hawajawa na msimu mzuri.

Ushindi wa kwanza baada ya mapumziko mafupi unaifanya Dortmund kukwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa Bundesliga, alama nne nyuma ya vinara RB Leipzig ambao baadae watacheza dhidi ya Union Berlin.

Author: Bruce Amani