Haaland atupia, Dortmund ikipigwa na Werder Bremen

Erling Braut Haaland ameendelea kuweka rekodi ya ufungaji katika klabu yake mpya ya Borussia Dortmund licha ya goli lake kutoisaidia Dortmund kushinda dhidi ya Werder Bremen baada ya kukubali kipigo cha goli 3-2 kwenye mchezo wa kombe la ligi.

Kinda Haaland, 19, aliingia kama mchezaji wa akiba mwezi Januari lakini tayari ameshafunga goli nane katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa.

Goli la jana linamfanya Haaland kufikisha goli 32 katika mechi 26 pekee, rekodi ya kipekee pia.

Haaland aliingia wakati Dortmund ikiongozwa 2-0 akagunga moja na kufanya matokeo kuwa 2-1 kwa magoli ya mapema ya Davie Selke na Leonardo Bittencourt ya kipindi cha kwanza kwa Werder.

Goli la tatu kwa Werder lilifungwa na Rashica wakati la pili kwa Borussia Dortmund likitiwa kimiani na Giovanni Reyna.

Matokeo hayo yanaifanya Dortmund kupoteza nafasi ya kushinda Kombe la Ligi kwani hata uwezekano wa kutwaa taji la Bundesliga sio rahisi kutokana na uwepo wa ushindani wa ligi yenyewe, Bayern Munich, Leipzig wanalitolea macho taji hilo.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments