Hadithi ya miaka 13 ya David Alaba yafikia ukomo Bayern Munich

David Alaba amethibitisha kuwa mwishoni mwa msimu huu ataondoka ndani ya klabu ya Bayern Munich baada ya kushindwa kuelewana juu ya mkataba mpya klabuni hapo. Kuondoka kwa kitasa huyo kinahitimisha hadithi ya takribani miaka 13 kwani alijiunga na miamba hiyo ya soka la Ujerumani mwaka 2008 ambapo ameshinda kila taji kubwa na kikosi hicho cha Bavarian.

Alaba, 28, amefunga goli 33 kwenye mechi 415 kwenye uzi wa Bayern, akiisaidia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2013 na 2020.

Hadithi imefika tamati. Swali ni wapi anaelekea katika umri wa miaka 28. Amekuwa akihusishwa kujiunga na timu mbalimbali barani Ulaya, Manchester United, Real Madrid, Paris St-Germain ni baadhi ya klabu ambazo zimeonyesha nia ya kumhitaji.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares