Hakuna matumaini ya kumpata mchezaji wa Cardiff City akiwa hai

Hakuna “matumaini yoyote” ya kumpata mchezaji wa kandanda wa klabu ya Cardiff City Emiliano Sala akiwa hai. Ni kauli ya afisa mmoja anayehusika na shughuli za uokozi.

Mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, na rubani walikuwa kwenye ndege hiyo ndogo ya kukodi ambayo ilipoteza mawasiliano wakati ikiwa katika eneo la Alderney katika visiwa vya bahari baina ya Uingreza na Ufaransa Jumatatu usiku. Mkuu wa Timu ya Utafutaji wa Angani ya Visiwa hivyo John Fitzgerald amesema “hata mtu ambaye yuko fit kabisa” angeweza kuwa hai majini kwa masaa machache tu. shughuli ya kutafita ndege hiyo iliyotoweka pamoja na waliokuwemo iliendelea tena leo.

Emiliano Sala alikamilisha uhamisho wake katika klabu ya Cardiff City Jumamosi

Sala inadaiwa alituma ujumbe wa sauti kwa njia ya Whatsapp kwa familia yake akisema “alikuwa na uwoga”. Vyombo vya habari Argentina vinaripoti kuwa alisema “niko kwenye ndege ambayo inaonekana kana kwamba itavunjika katika vipande vipande”. Wakati huo huo salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa kutokana na kutoweka kwa mchezaji huyo.

Author: Bruce Amani