Halaand aiweka Dortmund katika nafasi nzuri baada ya ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya Sevilla

Erling Braut Haaland aliendeleza makali yake ya ufungaji mabao katika Champions League wakati Borussia Dortmund ilipoyaweka pembeni matatizo yao ya ligi ya nyumbani na kuchukua udhibiti wa mechi yao ya hatua ya 16 dhidi ya Sevilla. Dortmund waliibuka na ushindi wa mabao 3 kwa 2 ugenini.

Lakini walijikuta nyuma kupitia bao la Suso ambalo lilipatikana baada ya mpira kumgonga Mats Hummels.

Mahmoud Dahoud alisawazisha kabla ya Haaland kupata bao lake la 17 katika mechi 13 za mashindano hayo na kuwaweka kifua mbele.

Kisha akafikisha la 18 muda mfupi baadae baada ya kuutumbukiza mpira wavuni kwa ustadi mkubwa. Luuk de Jong alifunga katika dakika za mwisho na kuwapa Sevilla matumaini kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Ujerumani Machi 9.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares