Harry Kane ashindwa kuonekana mazoezi Tottenham

Mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane ameshindwa kuonekana kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo mara baada ya muda wa mapumziko kumalizika ikielezwa kuwa ni sehemu ya kushinikiza kuondoka klabuni hapo.

Kane, 28, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester City huku yeye mwenyewe mara kadhaa akizungumza na Waandishi wa Habari amekuwa akieleza kuwa anahitaji kutoka Spurs kwenda kushinda mataji kwingineko

Mshambuliaji huyo alikuwa amepangiwa ratiba ya kufanyiwa vipimo vya Corona Leo Jumatatu Agosti 2 kabla ya kuanza rasmi mazoezi kesho Jumanne Agosti 3, mara baada ya mapumziko ya kushiriki michuano ya Euro 2020 kumalizika.

Inafahamika kuwa Mwenyekiti wa klabu Daniel Levy pamoja na kocha Nuno Espirito Santo hawako tayari kumuachia mshambuliaji bora wa msimu uliopita akiwa bao 23 ikiwa ni mara ya tatu baada ya 2015/2016, 2016/2017.

Akizungumza kwenye mazungumzo yake ya kwanza na Vyombo vya Habari, kocha mpya wa kikosi hicho Nuno alisema kuwa “Harry ni miongoni mwa wachezaji bora duniani, kila mmoja anatamani kuwa naye kwenye timu”, alisema kocha huyo wa zamani wa Wolves.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends