Harry Kane kuikosa LASK kutokana na majeruhi

Nahodha wa England na Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane atakosa mechi ya Europa Ligi dhidi ya LASK baada ya kupata majeruhi, inadaiwa kuwa huenda akawa sawa kwenye dabi ya wikiendi ijayo dhidi ya Arsenal.

Strika Carlos Vinicius, kiungo mshambuliaji Erik Lamela na mlinzi wa pembeni Sergio Regulion wote kuna mashaka endapo watatumika kwenye mechi ya leo Alhamisi nchini Austria.

Kane, 27, ana goli saba na assisti tisa katika mechi 10 za EPL. “Ana majeruhi lakini sitawaambia asili ya majeruhi yake, ila ana nafasi ya kucheza mechi ya Arsenal. Sihitaji kuogopa katika hili, kuna uwezekano mkubwa wa kucheza” amesema kocha mkuu wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends