Harry Kane sasa kubakia Tottenham

55

Nahodha wa kikosi cha Ligi Kuu England Harry Kane sasa atasalia ndani ya Tottenham Hotspur kufuatia klabu ya Man City kukata tamaa sawa na Daniel Levy kushikilia msimamo wake.

Manchester City walikuwa wanahitaji saini ya mshambuliaji huyo ambapo walikuwa na makubaliano ya awali ingawa msimamo wa Dany Levy ni ule ule

Licha ya ofa nzuri inayokadiliwa kufikia pauni milioni 150 bado Levy alikaa, kwa Kane mwenye umri wa miaka 28 na kuonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo kwa ajili ya kushinda mataji.

Kane alicheza mechi yake ya kwanza msimu huu kwenye ushindi wa Spurs wa goli 1-0 dhidi ya Wolves.

Author: Bruce Amani