Hatua ya mchujo Champions League yaja, nani kafuzu?

50

Spurs, Manchester City na Real Madrid zimejikatia nafasi katika duru ya 16 ya Champions League baada ya michuano ya Jumanne. Huku

Huku Bayern Munich, Juventus, na PSG zikiwa tayari katika hatua ya mtoano kabla ya michuano ya wiki hii, timu sita zinaweza kuangazia macho yao katika duru hiyo ya mchujo zikiwa zimebaki na mechi moja ya kucheza katika hatua ya makundi.

Nani kafuzu

Bayern Munich tayari walikuwa wametinga kutoka Kundi B, lakini wataungana na Spurs baada ya timu hiyo ya Jose Mourinho kupambana na kushinda 4 – 2 dhidi ya Olympiakos.

Sare ya Manchester City ya 1 -1 dhidi ya Shakhtar Donetsk ilitoka kuwapa tiketi ya kuwa kinara wa Kundi C.

Juventus tayari ilikuwa imepenya kutoka Kudi D, lakini ushindi wao wa 1 – 0 dhidi ya Atletico Madrid uliwahakikishia nafasi ya kwanza.

Bado kuna mechi za Makundi E – H, miongoni zikiwa ni Barcelona-Dortmund, Liverpool dhidi ya Napoli, Chelsea dhidi ya Valencia na Ajax dhidi ya Lille.

Mechi za mwisho za makundi zitachezwa Desemba 11 na 12

Author: Bruce Amani