Hawa hapa wachezaji 10 bora Ulaya walio chini ya miaka 23

Ukiwa unamtazama mchezaji mdogo anaonyesha kiwango bora huku akiwa na mwanga katika ukuaji wake ni jambo la heri. Kipindi hiki barani Ulaya kuna vipaji vingi vilivyo chini ya miaka 23 ambapo ukiwatazama unaona maisha ya baadae watafika mbali huenda pia tukashuhudia wakishindana kwenye tuzo kubwa duniani.

Ni wachezaji wengi vijana, lakini hapa Amani Sports News inakuletea makinda 10 bora Ulaya wenye umri china ya miaka 23 kwenye ligi tofauti tofauti wanaofanya vizuri na thamani kubwa.

10 Joe Gomez

Gomez ana umri wa miaka 22 anakipiga kunako vinara wa EPL Liverpool nafasi ya ulinzi. Kinda huyu ametunza kutoruhusu goli mechi 10 na amefungwa mechi 4.

Licha ya umri mdogo amewatoa magwiji kama Joel Matip na Lovren katika kikosi cha Majogoo wa Jiji la Liverpool.

  1. Gabriel Jesus

Umri miaka 22, klabu ya Manchester City nafasi ya ushambuliaji, strika huyu amekuwa na takwimu nzuri tangu ajiunge nayo.

Hakuna mchezaji yeyote wa Manchester City ambaye amefunga goli 5 kwenye Uefa lakini pia amegusa mipira mingi (39) ndani ya boksi la mpinzani.

Kiwango bora chake mara nyingi hufichwa na mkongwe Sergio Aguero ambaye amekuwa akianzishwa mara nyingi licha ya kuonyesha kiwango bora dhidi ya Real Madrid.

  1. Marcus Rashford

Rashford, 22, ameshahusika katika magoli mengi msimu huu 14 kuliko kinda yoyote mwenye umri wa chini ya miaka 23, EPL.

Marcus alihusika kwenye goli 11 kwenye michezo yote mikubwa kwa maana dhidi ya timu zilizo ‘top six’.

  1. Lautaro Martinez

Martinez huenda likawa jina jipya masikioni mwako lakini kunako Inter Milan ameshafunga goli 5 katika mechi 10 za Uefa msimu wa 2019/20 sawa na asilimia 50 ya goli zote.article image

Tangu Luis Suárez ameanza kusumbuliwa na majeruhi, Martinez amekuwa akihusishwa kama mbadala wa strika huyo wa Uruguay.

  1. Frenkie de Jong

Zao bora la Ajax iliyofanya vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/19 ambapo kama si juhudi za Tottenham Spurs huenda ingefika hata fainali.

De Jong, 22 anakipiga Barcelona, ni mchezaji mmoja tu anamzidi kwa kusukuma mipira ambaye ni Lionel Messi.

  1. Martin Odegaard

Odegaard, 21, amehusika kwenye utengenezaji wa nafasi 54, ndiye kinara katika umri wao wa chini ya miaka 23 La Liga.

Kinda huyo anakipiga kunako Real Sociedad ameshawavutia Barcelona na Atletico Madrid.

  1. Erling-Braut Haaland

Mwiba wa magoli pale Borussia Dortmund, akiwa na umri wa miaka 19 pekee tayari ameshafunga goli 10 kwenye Uefa, anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli hizo

Tangu alipojiunga na Dortmund kutokea RB Salzburg, Haaland amewasaulisha uwepo Pierre Emerick Aubameyang.

  1. Trent Alexander-Arnold

Licha ya kucheza nafasi ya ulinzi eneo la kulia mwa Uwanja kwenye kikosi cha Liverpool, Trent Alexander-Anord, 21, tayari ameshasaidia goli 10+ kwenye misimu miwili mfululizo.

Jamie Carragher alinukuliwa akisema ni mlinzi bora duniani wa pembeni huku sifa yake kubwa ni kupiga krosi ‘majalo’ anakumbusha enzi za David Beckham.

  1. Jadon Sancho

Zao la England linalotesa kule Borussia Dortmund akiwa na umri wa miaka 19.  Sancho amefunga na kutoa assiti katika mechi 9 kuliko mchezaji yeyote katika tano bora duniani.

Ameshaanza kuwatamanisha Manchester United, Madrid na Barcelona.

  1. Kylian Mbappé

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na Ufaransa amekuwa keki ya dunia hivi sasa, katika umri wa miaka 21 tayari ameshajitengenezea ufalme wake pale PSG.

Ametengeza goli 20 na kufunga goli 64 katika mechi 84, lakini pia Mbappe ameshatwaa ubingwa wa Ligue 1 na vilabu viwili tofauti (Monaco na PSG).

Hawa ndiyo vijana ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri wa viwango vyao katika timu na ligi wanazochezea.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments