Haya hapa maneno ya Nugaz baada ya kuachana na Yanga

Muda mfupi baada ya Yanga kuweka wazi kuwa haitaendelea kufanya kazi na aliyekuwa Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz kufuatia mkataba wake kumalizika klabuni hapo, Mhamasishaji huyo ametoa maneno ambayo sawa na kuwaaga mashabiki.

Itakumbukwa Leo mchana, Yanga iliweka wazi kuwa ndoa ya miaka miwili na Antonio Nugaz imefikia tamati na haitaendelea kufanya kazi pamoja.

Kupitia ukurasa wa Instagram Nugaz ameandika kuwa:-“Kwa udhati wa moyo wangu naomba niwashukuru kuanzia uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia Yanga kwa moyo mkunjufu na kujitoa kwangu.

“Mungu awabariki, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele brand, (nembo) ya Yanga.

“Wanachama,wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mmekuwa na mimi kwa moyo mmoja ahsanteni sana. Nawapenda sana na niatendelea kuwa nanyi.

“Tutaonana tena hivi karibuni. Insha Allah,”.

Kuondoka kwa Nugaz kunakamilisha usemi wa Waswahili kuwa “Ukiona kipa anapasha misuli wakati mechi inaendelea, vyovyote vile atakayetoka ni kipa vile vile” ikilandana na hili lilitokea, Haji Manara alitambulishwa siku chache zilizopita kabla ya Nugaz kuachana naye.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares