Hii hapa droo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania – ASFC

Droo ya Kombe la Shirikisho Tanzania katika hatua ya robo fainali imefanyika leo katika Makao Mkuu ya Azam TV ambapo miongoni mwa droo yenye mvuto ni kati ya Simba dhidi ya Azam FC.

Ratiba hiyo inaenda sawa na tarehe ya kuanza kwa michezo hiyo ambapo Juni 27 na 28 kutafanyika mechi hizo jijini Dar es Salaam.

Mchezo utakao kuwa wenye kuvuta hisia ni pamoja na pale bingwa mtetezi wa FA wa Azam Fc atakutana na Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa TPL.

Kagera Sugar itamenyana na Yanga.

Alliance itamenyana na Namungo huku Sahare All Stars ambayo ni timu pekee inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kutinga hatua ya robo fainali itamenyana na Ndanda

Mshindi wa mechi kati ya Simba na Azam atakutana na mshindi kati ya mechi ya Yanga na Kagera Sugar hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa Alliance na Namungo wao mshindi nusu fainali atamenyana na yule atakayeshinda mechi kati ya Ndanda na Sahare All Stars.

Mshindi wa mchezo wa fainali wa Kombe hili huwakilishi taifa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo huandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends