Hispania yabanwa na Misri Olimpiki Tokyo 2020

Timu ya Taifa ya Hispania imeshindwa kuliona lango hali kadhalika kwa timu ya taifa ya Misri katika sare tasa ya mtanange wa mashindano ya Olimpiki Tokyo 2020 yanayoendelea nchini Japan kufuatia kutofanyika mwaka Jana.

 

Hispania ambayo kabla ya mchezo huo ilikuwa inapewa kipaumbele cha kushinda kutokana na ubora wa kikosi hasa kinda ambaye alijumuishwa kwenye kikosi Bora cha Euro 2020, Pedri.

 

Pigo kwa kocha wa Hispania sio sare waliyoipata kwa Misri pengine ni mara mbili zaidi baada ya kuumia kwa kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Dani Ceballos kwa enka ambaye kabla ya kutoka alionyesha kandanda safi.

 

Wakati mlinzi wa zamani wa West Brom Ahmed Hegazi akisimama kidete kuhakikisha usalama wa eneo la ulinzi uko asilimia 100.

 

Mbali na Pedri, wachezaji wengine ambao walianza kwenye kikosi cha leo walikuwa kwenye michuano ya Euro ni Mikel Oyarzabal, Dani Olmo, Pau Torres na Eric Garcia.

 

Hispania waliondolewa na mabingwa Italia kwenye mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kukamilika za Euro 2020.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares