Hispania yalamba alama tatu kwa kuifunga Kosovo 3-1

Taifa la Hispania limemaliza mechi tatu za awali za kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 kwa kuitandika 3-1 timu ya taifa ya Kosovo katika mchezo uliopigwa Jana Jumatano huku kiungo mshambuliaji wa Manchester City Ferran Torres akifunga bao moja.

Dani Olmo wa RB Leipzig alifungua akaunti ya magoli akitumia vyema pasi ya beki wa Barcelona Jordi Alba kunako dakika ya 34 ya mchezo.

Torres aliongeza bao la pili dakika mbili baadae kabla ya Kosovo kufunga bao moja kupitia kwa Besar Halimi na baadaye Gerard Moreno akafunga akaunti ya magoli kwa goli la tatu na kufanya matokeo kuwa 3-1.

Matokeo hayo yanaifanya Hispania kuwa kinara wa kundi B alama saba kwenye mechi tatu.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares