Hizi ndizo timu 16 zilizotinga hatua ya mchujo

Hatimaye mechi za hatua ya makundi ya Champions League zimefikia kikomo na sasa ni rasmi nani ametinga hatua ya hatua ya timu 16 za mwisho. Kufuatia matokeo ya Jumatano usiku ya mechi za mwisho za makundi, hizi ndizo timu zilizojikatia tiketi ya kucheza hatua ya mchujo: FC Barcelona, Napoli, Borussia Dortmund, Liverpool, Valencia, Chelsea, RB Leipzig, Olympique Lyonnais, Real Madrid, PSG, Man City, Bayern, Tottenham, Atalanta, Juventus na Atletico Madrid.

Shirikisho la kandanda UIaya – UEFA litafanya droo ya hatua ya mchujo Jumatatu Desemba 16  2019 kufahamu ratiba kamili ya mechi zitakazofuata. Michezo hiyo itachezwa kuanzia February 18/19 & 25/26 2020 kwa mechi za kwanza na marudiano ni Machi 10/11 & 17/18 2020.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends