Homeboyz Watoa Sare na Gor Mahia

25

Kakamega Homeboyz wamelazimisha sare ya bao 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya mtanange uliopigwa Leo Jumamosi dimba la Kasarani Jijini Nairobi.

Mabao kwenye mechi hiyo yamefungwa na Samuel Onyango ambaye alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake ya Gor Mahia akimalizia pasi ya Benson Omala kabla ya Michael Karamor kusawazisha na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare ambayo siyo matokeo mazuri kwa Kakamega Homeboyz.

Matokeo hayo yanaifanya Kakamega Homeboyz kufikisha pointi 60 alama nne dhidi ya Tusker FC ambao watakuwa na mchezo Jumapili dhidi ya kibonde Nzoia Sugar wakati Gor Mahia wakiwa nafasi ya tano alama 38.

Author: Asifiwe Mbembela