IAAF yafanya mabadiliko mashindano ya Diamond League

Shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF, limetangaza kuwa, kuanzia mwaka 2020, mashindano ya mbio za Mita 200 na 3,000 kuruka viunzi na maji, hayatajumuishwa katika mashindano ya Diamond League.

Kila mwaka kuna mashindano 15 ya Diamond League na sasa mashindano 12 ya riadha ndio yatakoyosalia.

IAAF inasema lengo ni kuwezesha mashindano hayo kusalia na mashindano ambayo yatakuwa na ushindani mkubwa na kutumia muda mfupi na kuwavutia watazamaji na mashabiki.

Mashindano ya IAAF Diamond League yalianza mwaka 2010, na kuchukua nafasi ya IAAF Golden League ambayo yalianza mwaka 1998.

Wanariadha kutoka Marekani, Kenya, Jamaica na Ethiopia, yameendelea kufanya vema katika mashindano haya.

Author: Bruce Amani