Ibrahimovic arejea Milan akitokea Marekani

178

Staa wa Sweden aliyewahi pia kuichezea Manchester United Zlatan Ibrahimovic amerejea AC Milan katika dili la miezi sita kukitumikia kikosi cha timu hiyo huku kukiwa na kipengele cha kuongeza msimu mwingine endapo atafanya vizuri.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 38 alikuwa mchezaji huru tangu aondoke LA Galaxy inayoshiriki ligi ya kuu ya Marekani MLS.

Mabingwa wa zamani wa Ulaya AC Milan awali walithibitisha kuwa Ibrahimovic angewasili leo Januari 2 kufanya vipimo vya afya sambamba na kujiunga na timu hiyo rasmi.

“Narejea sehemu niipendayo, Klabu ninayoiheshimu na katika Mji(Milan) niupendayo naamini nitafanya kazi bora kama kawaida yangu”, alisema Ibra baada ya kujiunga na timu hiyo.

Ibrahimovic amewai kuwa Milan ndani ya Seria A msimu wa 2010-2012 ambapo alifunga goli 42 katika michezo 61 ya Ligi ndani ya klabu hiyo.

Milan wamekuwa wakisuasua tangu watwae ubingwa wao wa mwisho mwaka 2011 huku urejeo wa Zlatan ukilenga kuimarisha eneo la ushambuliaji wa timi hiyo, mpaka Sasa wako nafasi ya 11 kwa alama 21 katika michezo 17.

Author: Bruce Amani