Ibrahimovic kitanzini AC Milan

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden na AC Milan Zlatan Ibrahimovic yuko kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho.

Mkataba wa sasa wa Zlatan Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 39, unakamilika Juni, akiwa amefunga goli 15 msimu huu ndani ya Serie A.

Nyota huyo wa zamani wa Paris St-Germain, Manchester United, Barcelona na Inter Milan wiki iliyopita alirudi kwa mara ya kwanza kwenye majukumu ya timu ya taifa baada ya kukaa kando kwa miaka mitano.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares