Ibrahimovic Kuwa Nje ya Uwanja Miezi 8

118

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden na AC Milan Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi nane akifanyiwa upasuaji wa goti.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 40, ameisaidia Milan kushinda taji la Serie A kwa mara ya kwanza tangia mwaka 2011 ambapo sasa atauguza jeraha baada ya upasuaji.

Mkataba wa strika huyo matata wa zamani wa Manchester United, Barcelona na Inter Milan unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini alishaonyesha matamanio ya kuendelea kusalia Milan kwa msimu mmoja zaidi.

Kwa msimu huu ameanza mechi 11 ambapo amefunga magoli 8 na mara nyingi amekuwa akisumbuliwa na majereha ya hapa na pale.

Author: Bruce Amani