Icardi aipa Inter ushindi dhidi ya mahasimu Milan

Mauro Icardi, nahodha wa Inter Milan alifunga bao la ushindi katika dakika za majeruhi dhidi ya mahasimu wao wa jiji AC Milan katika dimba la San Siro kwenye mtanange wa ligi kuu ya kandanda Italia – Serie A

Debi hiyo ya 222nd Milan ilionekana kuwa inaelekea kukamilika kwa sare tasa kabla ya mshambuliaji huyo wa Argentina kufunga bao la kichwa kutokana na krosi ya Matias Vecino.

Inter – ambao ilibidi wacheze bila ya kiungo Radja Nainggolan aliyetoka uwanjani baada ya kuumia, walistahili ushindi huo lakini ulikuwa mchuano ambao haukusisimua..

Icardi – aliugusa mpra mara 15 pekee katika mechi nzima wakati Mateo Musacchio wa AC Milan akifunga mabao ambayo yalifutwa kwa sababu alikuwa ameotoea

Ushindi huo wa debi unaiweka Inter katika nafasi ya tatu na pointi 19 mbili nyuma ya nambari mbili Napoli, huku AC Milan ikisalia katika nafas ya 12 ya msimamo wa ligi

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends