Idrissa Gueye aondoka Everton na kujiunga na PSG

60

Paris St Germain wamemsaini kiungo wa Everton Idrissa Gueye. Msenegal huyo mwene umri wa miaka 29 amesaini mkataba wa miaka minne na mabingwa wa Ufaransa.

Alijiunga na Everton mwaka wa 2016 akitokea Aston Villa na akaichezea klabu hiyo ya Merseyside mechi 108. Inakisiwa kuwa PSG wametoa karibu pauni milioni 30 kuipata saini ya mchezaji huyo. Staa huyo aliyefika katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika – Afcon 2019 nchini Misri akiwa na timu yake ya Senegal pia alikuwa akiwindwa na Manchester United. “Nina furaha kubwa sana kujiunga na klabu hii.” Gueye aliiambia PSG mara baada ya kukamilisha uhamisho wake. Aliichezea Lille ya Ufaransa misimu saba kuanzia 2008 hadi 2015 kabla ya kuhamia Premier League ya England

Author: Bruce Amani