Ighalo aipa Nigeria ushindi mwembamba dhidi ya Burundi

52

Washindi mara tatu na mabingwa wa mwaka wa 2013 Nigeria walipata ushindi mgumu wa 1 – 0 dhidi ya Burundi ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezaji aliyeingia kama nguvu mpya katika kipindi cha pili Odion Ighalo alifunga bao hilo la pekee kunako dakika ya 77 mjini Alexandria aliposukuma wavuni shuti maridadi iliyomzidi maarifa kipa wa Burundi Johathan Nahimana.

Burundi – inayoorodheshwa ya chini kabisa katika mashindano hayo – ilipiga mtambaa panya katika kipindi cha kwanza kupitia kichwa safi cha beki wao Frederic Nsabiyumva.

Author: Bruce Amani