Ighalo anataka kuongezwa kandarasi yake ya mkopo Manchester United

48

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo anaamini kandarasi yake ya mkopo klabuni hapo itadumu mpaka pale msimu huu utakapomalizika.

Straika huyo raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na Mashetani Wekundu kwa mkopo mwezi Januari akitokea China katika klabu ya Shanghai Shenhua ambapo kandarasi yake inatamatika Mei 31.

Mabosi wa EPL wanatumaini kurejesha ligi mwanzoni mwa mwezi Juni, muda ambao hata ligi ya China; Super ligi inategemewa itarejea, Ighalo anaweza akarudi katika klabu mama ya Shanghai.

“Nitapendelea kumalizia msimu nikiwa hapa, lakini kama itawezekana,” alisema Ighalo.

“Nilikuwa katika kiwango kizuri, muonekano mzuri na kufunga magoli lakini tumesimamishwa kwa zaidi ya mwezi mmoja. Natamani kufanya kila linalowezekana kucheza tena na tutarejea kwa ubora zaidi.

Tayari alikuwa amefunga goli 4 katika michezo 8 ambayo amecheza katika mashindano yote ya United, miongoni mwa mechi hizo ni ile ya ushindi wa goli 5-0 dhidi ya LASK uliopigwa 12 Machi, siku moja kabla ya EPL kusimamishwa mpaka sasa kutokana na Covid-19.

Author: Bruce Amani