Ighalo kuendelea kuichezea timu ya ndoto zake, Manchester United

Mshambuliaji wa Manchester United na Nigeria Odion Ighalo ameongeza kandarasi ya mkopo ndani ya United akitokea Shanghai Shenhua ambapo hivi sasa kandarasi hiyo inatamatika Januari 2021.

Ighalo, 30, alijiunga na United mwezi Januari akitokea katika ligi kuu nchini China maarufu kama (Super league) katika klabu ya Shanghai Shenhua ambapo mkataba wake kwa mkopo ulitakiwa kuisha Mwezi Mei 31.

Hakuna kipengele cha kumnunua moja kwa moja strika. “Bila shaka atatimiza ndoto yake hapa ya kushinda kile alichokianzisha na huenda pia akashinda mataji nasi” alisema kocha mkuu wa Mashetani Wekundu Ole Gunnar Solskjaer.

“Shanghai Shenua wametupa ushirikiano mkubwa sana ambao hatukuutegemea awali, hasa kumruhusu kucheza katika klabu ya ndoto zake”.

Ighalo tayari ameshafunga goli nne katika mechi nane ndani ya Old Trafford, miongoni mwa goli zake ni lile alilofunga dhidi ya LASK uliopigwa Marchi 12 ambapo United alishinda goli 5-0.

Ligi Kuu nchini England imekusudia kuanza kuchezwa tena Juni 17 baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na hofu ya virusi vya Corona.

United wapo nafasi ya tano, pointi tatu nyuma ya timu iliyonafasi ya tatu Chelsea huku michezo tisa ikiwa imesalia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends