Inashangaza kidogo ukilitafakari hili la Simba

271

Hii inatokea Tanzania tu bila shaka. Kwa uchunguzi wa kawaida tu utabaini kwamba Tanzania hakuna “u’serious” kwenye mpira wa miguu.

Inakuwaje Simba inamuachia kiungo bora msimu uliopita ndani ya klabu yao? James Kotei. Wakati hata jibu haujapata unasikia Haruna Niyonzima ameaga Msimbazi.

Ifahamike! Mchezaji kuachwa sio shida bali kuachwa mchezaji bora, kuna shida hapo. Ubora aliupatia wapi kama sio kucheza uwanjani. Wengine wanadai ni ripoti ya Mwalimu kweli kocha gani ambaye atakubali Kotei aondoke, kwa Haruna Niyonzima naweza sema sawa hakuwa na msimu mzuri lakini Kotei? Mh

Real Madrid ya Hispania ina kauli yao wanasema “Ili uwe bora lazima uwe na wachezaji bora” wakimaanisha, Kama unashindwa kuwatuza wachezaji bora kwenda kwenye vilabu vingine ni vigumu kuwa bora.

Tatizo kubwa ninaloliona mimi ni kuingiza siasa kwenye soka. Baadhi ya watu wamekuwa wakitengeneza hela kila usajili unapofanyika. Ni vigumu kuelewea kinachofanyika kwenye soka la Tanzania katika zama hizi za ustaarabu.

Simba ilifika robo fainali ligi ya mabingwa Afrika licha ya kutokuwa na uzoefu, kushiriki kwa Kotei, Niyozima nk kungetengeza muunganiko(chemistry) wenye tija.

Sasa kama kila mwaka unasajili ina maanisha kila mwaka utakuwa unajenga timu badala ya kwenda kushindana.

Wanasimba hili limekaaje kwenu?

Author: Asifiwe Mbembela