Infantino achaguliwa tena kuwa rais wa FIFA

Gianni Infantino leo amechaguliwa tena kuwa rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kwa muhula mwingine wa miaka minne utakaomaliza mwaka 2023. Infantino mwenye umri wa miaka 49 ambaye ni raia wa Uswisi amechaguliwa kwa kura ya sauti kwa sababu ya kuwa mgombea pekee katika kongamano la FIFA linalofanyika mjini Paris, Ufaransa.

Infantino amekuwa rais wa FIFA tangu alipochaguliwa mwaka 2016 kumalizia muhula wa mtangulizi wake Sepp Blater ambaye anatumikia marufuku ya miaka sita ya kutojihushisha na masuala ya kandanda.

Infantino amewaambia wajumb ewa kongamano la FIFA kuwa shirikisho hilo limepiga hatua kubwa tangu lilipitumbukia kwenye kashfa ya za rushwa zilizopelekea kuondoka madarakani kwa Blatter mwaka 2015

Author: Bruce Amani