Infantino apendekeza Afcon iandaliwe kila baada ya miaka 4

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino amependeza michuano ya kuwania ubingwa baina ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, ichezwe kila baada ya miaka minne, badala ya miwili ilivyo sasa.

Infatino ametoa kauli hii hivi leo, mjini Sale, nchini Morocco wakati akikutana na wakuu wa vyama vya soka kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Rais huyo wa soka duniani, ameongeza kuwa iwapo hii litafanyika basi michuano hii itasaidia kuongeza mapato lakini pia kivutio kikiwa duniani.

Wazo hili, bila shaa litaungwa mkjono na wamiliki wa vlabu barani Ulaya, ambao wamekuwa wakisikitika kuwakosa baadhi ya wachezaji wa Kiafrika ambao hurudi nyumbani kuzichezea nchi zao.

Pamoja na hilo, infatino anapendekeza kuwa michuani ya vijana, chini ya miaka 16, 18 ichezwe kila baada ya miaka miwili.

Aidha, amesema kuwa, bado bara la Afrika linahitaji msaada katika maeneo ya waamuzi, miund mbunu na kuandaa mashindano mbalimbali, ili kuinua michuano hii.

Author: Bruce Amani