Infantino apendekezwa kuwa mwanachama wa IOC – Bach

51

Rais wa FIFA Gianni Infantino amependekezwa kuwa mwanachama wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC, lakini kiongozi wa Mchezo wa Riadha Duniani Sebastian Coe atahitajika kusubiri kutokana na mgongano wa maslahi. Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa IOC Thomas Bach.

FIFA na Shirikisho la Riadha Duniani, mashirika yanayosimamia michezo miwili mikubwa kabisa katika Olimpiki, wamekuwa bila uwanachama tangu marais wao wa zamani Sepp Blatter na Lamine Diack walipoondoka katika IOC mwaka wa 2015.

Bach amesema Infantino amependekezwa kwa uchaguzi katika kikao chao kijacho Januari pamoja na mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Tennis David Haggerty na Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Japan Yasuhiro Yamashita.

“Tulimtaka Coe awe mwanachama wa IOC kama rais wa mojawapo ya michezo yetu muhimu ya Olimpiki,” alisema Bach. “Tangu wakati huo, tupo katika mashauriano ya karibu nay eye na tangu wakati huo tumeangazia kitisho cha kuwepo mgongano wa maslahi anayoweza kuwa nayo.” Ameongeza Bach.

Author: Bruce Amani